Mozilla haina malipo kwa susho, uboreshaji au msaada wa kiufundi, na haiidhinishi kampuni yoyote ambayo inafanya hivyo. Makampuni ambayo yanauliza malipo au maelezo ya kibinafsi kwa ajili ya kufunga, kuhuisha au kutoa msaada kwa Firefox au Thunderbird hazishirikiani na Mozilla na ziepukwe.
Table of Contents
Ulaghai wa kawaida wa msaada wa kiufundi
- Maonyo ya virusi ambazo hukuambia kipiga simu, kushusha programu au kuruhusu scan za virusi.
- Makampuni ambayo kutumia majina ya bidhaa ya Mozilla na nembo ili kukulipisha kwa ajili ya kufunga, fixing na kuhuisha Firefox au Thunderbird.
- Simu kutoka "wawakilishi ya Mozilla" kukushinikiza katika kulipa kwa ajili ya huduma au kupata kufikia kompyuta yako.
Ukijikuta katika yoyote ya ulaghai hizi, tembelea Federal Trade Commission (USA) au Econsumer.gov (international).
Kujikinga na ulaghai
- Tembelea tovuti rasmi ya Mozilla Support (https://support.mozilla.org) au rasilimali nyingine zinzotambuliwa kwa masuala yote ya msaada wa kiufundi. Hakuna makampuni mengine msaada ya kiufundi iliyopitishwa na Mozilla,
na kampuni nyingine yoyote ambayo inarumia jina Mozilla au nembo ya kudai uhusiano na Mozilla inapaswa kuripotiwa hapa.
- Mozilla hatoi msaada wa simu. Usipige simu au kutoa taarifa kwa mawakala wakidai kuwakilisha Mozilla.
- Shusha programu za Mozilla kutoka vyanzo rasmi tu.
- Ukurasa rasmi wa kushusha Firefox
- Ukurasa rasmi wa kushusha Firefox Thunderbird
- Wakati kushusha chochote kilicho na nembo ya Firefox kwenye simu yako au tablet, kagua maelezo ya developer na kuhakikisha kuwa kweli ni iliyotolewa na Mozilla.
Kuripoti ukiukaji alama ya biashara
Saidia kusimamisha scammers. Ukiona wengine wakitumia jina au alama ya Firefox au Thunderbird ili kuwakilisha Mozilla, wasilisha ripoti ya udanganyifu.