Njia rahisi ya kupata ilianza ni remix moja ya miradi starter kupatikana kwenye tovuti ya Thimble.
Bomba kifungo cha Remix katika mwanzo wa mradi. Utaona panei zifuatazo:
- Paneli ya kushoto inaonyesha faili katika mradi huo. Kwa mfano, unaweza kuona faili moja ya HTML, moja ya CSS na nyingine ya Javascript. Ukibonyeza mafaili mbalimbali, inabadilisha kile kinachoonekana katika paneli nyingine mbili.
- Paneli ya katikati inaonyesha kificho ya faili yoyote iliyochaguliwa.
- Paneli ya kulia inaonyesha hakikisho ya vipi ukurasa itakua kama kwenye kivinjari au simu ya mkononi.
Katika kila moja ya tengenezo za kwanza, paneli ya kulia inaweza badilishwa kutazama Mafunzo ya mradi. Bonyeza neno "Tutorial" katika baa ya kijivu juu ya kidirisha la hakikisho kuona hatua kwa hatua maelekezo ya jinsi ya ku-remix mradi. Usisahau, unaweza remix chochote kilichotengenezwa na Thimble, hivyo kama unaweza kuona kitu kimeundwa na wengine ambayo wewe pia wataka kufanya, bomba kifungo cha Remix na kuona ni jinsi gani walifanya hivyo!